1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RIYADH: Nchi za Kiarabu zatafuta ufumbuzi wa amani

29 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCET

Viongozi wa nchi za Mashariki ya Kati wanaendelea na majadiliano yao katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Nchi za Kiarabu mjini Riyadh.Viongozi hao wanatazamiwa kuzindua rasmi mchakato wa amani uliokwama.Nchi za Kiarabu zinapendekeza kuwa na amani na Israel na badala yake Israel iondoke kutoka maeneo iliyovamia katika vita vya mwaka 1967.Mpango huo pia unatoa wito wa kuundwa taifa la Palestina na kuruhusu wakimbizi wa Kipalestina kurejea nyumbani.Israel iliukataa mpango huo miaka mitano iliyopita,lakini wadadisi wa kisiasa wanasema,safari hii kuna ishara za matumaini kutoka Israel.