RIYADH: Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel, awasili Saudi Arabia | Habari za Ulimwengu | DW | 04.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RIYADH: Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel, awasili Saudi Arabia

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel, amewasili mjini Riyadh, Saudi Arabia, ambacho ni kituo cha pili cha ziara ya siku nne Mashariki ya Kati.

Kabla ya kuondoka kuelekea Saudi Arabia, Bibi Angela Merkel alishauriana na Katibu wa Umoja wa nchi za Kiarabu, Amr Moussa, mjini Cairo.

Bi Angela Merkel jana alikuwa na mashauriano na Rais wa Misri, Hosni Mubarak kuhusu mazungumzo ya amani kati ya Israil na Palestina.

Viongozi hao walisisitiza haja ya kuwepo mkakati wa pamoja wa kimataifa kufufua mazungumzo ya amani kati ya pande hizo mbili.

Bibi Angela Merkel, ambaye nchi yake inashikilia uenyekiti wa Umoja wa Ulaya, anatarajiwa pia kutembelea Muungano wa Mataifa ya Kiarabu, na Kuwait.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com