1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya UNAIDS-Watu millioni 33 wanaishi na virusi vya ukimwi.

Jane Nyingi12 Januari 2009

Ripoti ya hivi punde ya shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu ukimwi-UNAIDS, inakadiria kuwa watu millioni 33 duniani wanaishi na virusi vya HIV huku millioni 22 wakiwa kutoka barani la Afrika.

https://p.dw.com/p/GWdJ
ujumbe kuhusu ugonjwa wa ukimwi,BotswanaPicha: J. Sorges

Lakini baadhi ya mataifa ya bara hilo yamepiga hatua katika kupunguza maambukizi ya virusi hivyo huku mengine idadi ya walioambukizwa virusi vya HIV ikizidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo mabadiliko katika tabia za ngono nchini Rwanda na Zimbabwe zimesadia katika kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya HIV.Hatua ya vijana kutoka Burkinafaso, Ethiopia, Ghana, Malawi, Uganda na Zambia kusuburi kwa muda mrefu bila kujihusisha kigono pia imesadia katika kupunguza maambukizi.

Wanaharakati wa kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi pia wamechukua mwelekeo mpya kwa kujifahamisha zaidi kuhusu ugonjwa huo,kutathmini hali katika sehemu za mashinani hasa kwa kujua wenyeji walio na virusi vya ukimwi na kutafuta mbinu za kuwasadia.

Rwanda imeorodheshwa miongoni mwa matiafa 10 ambayo yameathiriwa zaidi na janga la ugonjwa wa ukimwi.Ni kutokana na hali hii ambapo serikali ya Rwanda imetambua matatizo yanayotokana na janga hilo na kuonyesha kujitolea kwake katika kutoa tiba na kuzuia maambukizi zaidi ya ukimwi.

Miongoni mwa juhudi zake zilizofanikiwa ni katika kuwahusisha wanaume kuzuia kusambaza virusi vya ukimwi kutoka kwa mama hadi mtoto.

Daktari Anita Asiimwe ,katibu mkuu wa tume ya kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchini Rwanda anasema na namnukuu" nikiangalia miaka iliyopita,ni asilimia 6 pekee ya wanaume waliokuwa wakiandamana na wake zao kwenda zahanati, lakini hivi sasa tarakimu hizo zimefikia asilimia 64,mwisho wa nukuu".

Kutokana na hayo,hofu iliotokana na ugonjwa wa ukimwi imepunguua na idadi ya wanawake wanakwenda kwenye zahanati kupima afaya zao kabla ya kujifungua imeongezeka.Dakta Assimwe nchini Rwanda anasema wanawake hutaraji baada ya kujua hali zao wanaweza kuwategemea waume zao katika kukabiliana na ugonjwa huoa na athari zake.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali,kiwango cha maambukizi ya virusi vya HIV nchini Rwanda kwa asilimia tatu tangu mwaka jana,hii ni kutoka asilimia 7 mwaka wa 200.Karibu asilimia 90 ya watoto wanaozaliwa na akina mama waliona virusi vya ukimwi, huwa hawana virusi hivyo,hii ikiwa hatua kubwa na serikali ya rwanda katika muda wa miaka miwili.

Ama Taarifa kutoka Kenya si za kuridhisha.Uchunguzi wa mara mbili uliofanywa unaonyesha kuwa maambukizi ya virusi vya HIV yameongezeka.Kwa mujibu wa ripoti ya afya ya 2003 ambayo ni ya hivi karibuni kufanywa kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kimefikia asilimia 6.7.Uchunguzi mwingine ulofanywa mwaka jana umeonyesha maambukizi yameongezeka kwa asilimia 7.8 kufikia mwisho wa mwaka huo.

Wataalamu wa kiafya wanasema mikakati iliyowekwa na serikali ya Kenya kukabiliana na ugonjwa huo imeshindwa kulenga kundi fulani la watu ambalo linasambaza kwa haraka ugonjwa huo na kwa hivyo kuendelea kuzungumzia tu kuhusu kuanzishwa vituo vya upimaji kwa hiari virusi vya Ukimwi vilinavyojulikana kwa jina la VCT kwa hakutoshi, bali kampeni kabambe ya ziada kuuelimisha umma inahitajika.