1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ripoti ya shirika la Umoja wa mataifa la UNDP

Oummilkheir27 Novemba 2007

Afrika ,kusini mwa jangwa la Sahara lakabiliwa na kitisho cha madhara ya kuzidi hali ya ujoto duniani

https://p.dw.com/p/CTpK
UkamePicha: AP

Ripoti ya mwaka ya shirika la maendeleo la Umoja wa mataifa –UNDP inazungumzia imechapishwa leo hii mjini Geneva.Ripoti hiyo inazungumzia madhara yanayotishia maisha ya wakaazi wa Afrika kutokana na kuzidi hali ya ujoto duniani.

“Waafrika hawana njia ya kujikinga dhidi ya matukio mabaya mno ya hali ya hewa na waneweza kuathirika vibaya sana na kuzidi hali ya ujoto duniani,hata kama bara lao si miongoni mwa yale yanayochafua mno mazingira.

Mabadiliko ya hali ya hewa yataliathiri vibaya sana eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara,na kusababisha madhara yatakayoendelea kuanzia kizazi kimoja au chengine”Hayo yametajwa katika ripoti ya mwaka ya shirika la maendeleo la umoja wa mataifa-UNDP iliyochapishwa hii leo mjini Geneva.

Kiwango cha joto kinapopanda barani Afrika,mavuno yanaharibika na watu wanakufa kwa njaa,au wakinamama na wasichana wanaingia njiani kwa muda mrefu kutafuta maji.

Kinyume chake,ripoti ya shirika hilo la umoja wa mataifa inasema,katika nchi tahiri,suala la mabadiliko ya hali ya hewa hutatuliwa kimsingi kwa kupunguza kiwango cha chombo cha kupima joto,msimu mrefu na wa joto wa kiangazi na kadhalika.

Wanaoathirika zaidi na ukosefu wa hali ya usawa majanga mfano dharuba,mafuriko na ukame yanapozuka,ni wakaazi wan chi maskini za dunia .Lakini Afrika kusini mwa jangwa la Sahara,ambako asili mia 40 ya watu wanaishi kwa chini ya dala moja kwa siku na wengine sawa na hao wanaishi kwa dala mbili kwa siku,adhari ni kubwa zaidi.

Kwa mujibu wa waratibu wa ripoti hiyo,kati ya wakaazi milioni 720 wa eneo hilo,watu kati ya milioni 70 hadi milioni 250 huenda hali zao za maisha au matumaini ya kujiendeleza yakatoweka hadi ifikapo mwaka 2020,kwaajili ya madhara ya kuzidi hali ya ujoto ulimwenguni.

Hali ya hewa inapovurugika,mazao ya kilimo yanaangamia na kusababisha ukosefu wa chakula bora na watoto hawakui vizuri.

Watoto wanaozaliwa katika kipindi cha ukame,mfano nchini Ethiopia na Kenya wanasumbuliwa zaidi na ukosefu wa chakula bora na hawakui vizuri.

Nchini Niger mafuriko ya mwaka huu yamesababisha vidimbwi vya maji ambayo mpaka leo mbu wanazaliana na kusababisha maradhi.

Shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP linakadiria hadi ifikapo mwaka 2060,ikiwa hali ya ujoto itaongezeka kwa digrii mbili nukta 9 na mvua kupungua kwa asili mia 4,basi pato la kila mkaazi mmoja wa eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara litapungua kwa robo.

Eneo hilo kwa jumla,ripoti inafafanua, linatoa moshi haba kabisa wa Carbon Dioxide kupita jimbo la Marekani la Texas kwa mfano.

“Kwao wao,mataifa tajiri yanabidi yawajibike zaidi na kuitumia fursa ya mkutano wa kimataifa wa Bali,mwezi ujao,kuhimiza ushirikiano wa kimataifa.Mkutano huo utasaka mkakati wa kufuatwa,kupunguza moshi wa viwandani- itifaki ya Kyoto itakapomalizika mwaka 2012.

Lakini serikali za Afrika nazo pia zinapaswa ziwajibike,ripoti hioyo inasema,kwa kuwasaidia raia kukabiliana na majanga hayo ya kimaumbile.

Ripoti ya shirika la umoja wa mataifa ya UNDP imezitaka nchi za Afrika ziwekezee katika kujenga ghala za kuhifadhi vyakula na maji katika maeneo ya mvua kubwa.Ripoti hiyo inashauri pia iimarishwe bima ya wakulima na watu wasiojimudu kuweza kukabiliana na majanga yanayosababishwa na hali ya hewa.