Rangoon. Wito watolewa kufanya maandamano duniani kupinga utawala wa kijeshi wa Burma. | Habari za Ulimwengu | DW | 04.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Rangoon. Wito watolewa kufanya maandamano duniani kupinga utawala wa kijeshi wa Burma.

Makundi ya haki za binadamu yametoa wito wa kufanyika siku ya maandamano duniani kupinga matumizi makubwa ya nguvu dhidi ya maandamano ya amani nchini Burma. Mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Amnesty International na Human Rights Watch yamejiunga na shirika la Crisis Action katika wito wa kuchukuliwa hatua Jumamosi ijayo kuhusiana na matumizi ya nguvu yaliyotumiwa na utawala wa jeshi nchini Burma, ambapo kiasi cha watu 13 wameuwawa na zaidi ya wengine 1,000 wamekamatwa.

Matukio yatafanyika katika nchi kadha ikiwa ni pamoja na Australia , Canada, Ufaransa, India , New Zealand , Uingereza na Marekani. Utawala wa kijeshi wa Burma umeongeza mbinyo dhidi ya watu wake jana Jumatano , ukionya kuwakamata watu zaidi baada ya msako uliofanyika wiki iliyopita, wakati umoja wa Ulaya ukikubali kimsingi kuwaadhibu watawala hao wa kijeshi kwa kuwawekea vikwazo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com