RAMALLAH: Wito kukomesha mapigano kati ya Fatah na Hamas | Habari za Ulimwengu | DW | 19.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RAMALLAH: Wito kukomesha mapigano kati ya Fatah na Hamas

Rais wa Wapalestina,Mahmoud Abbas na Waziri Mkuu Ismail Haniya wametoa mwito wa kusitishwa mapigano kati ya makundi hasimu Hamas na Fatah. Hadi hivi sasa,juhudi zote za kutaka kukomesha umwagaji wa damu,hazikufanikiwa.Watu 54 wameuawa katika mapigano ya siku tano kati ya makundi hayo hasimu.Mapigano hayo yamehatarisha misingi ya serikali ya umoja wa kitaifa,iliyoundwa na makundi hayo mawili ya Wapalestina,miezi miwili iliyopita tu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com