RAMALLAH: Juhudi za Hamas na Fatah kudhibiti machafuko | Habari za Ulimwengu | DW | 20.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

RAMALLAH: Juhudi za Hamas na Fatah kudhibiti machafuko

Maafisa wa Fatah na Hamas wamekutana kwenye Ukanda wa Gaza kwa azma ya kudhibiti machafuko yanayozidi kuongezeka kati ya makundi hayo mawili hasimu ya Kipalestina.Huo ni mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu kupata kufanywa baada ya majuma kadhaa.Kinyanganyiro cha madaraka kati ya Hamas na Fatah,kilichochea mapigano ya mwezi huu,kati ya wanamgambo na kusababisha vifo vya si chini ya watu 19.Majadiliano ya majuma kadhaa yaliofanywa kati ya Rais Mahmoud Abbas wa Fatah na kundi la Hamas katika juhudi ya kuunda serikali ya umoja na kukomesha mapigano,hadi hivi sasa yameshindwa kufanikiwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com