1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani ziarani Afghanistan

Mohamed Dahman/ZPR 16 Oktoba 2011

Rais Christian Wulff wa Ujeruamani anafanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan. Hii ni ziara ya kwanza kuwahi kufanywa na mkuu wa nchi wa Ujerumani kwa Afghanistan katika kipindi cha miaka 44.

https://p.dw.com/p/RrCb
Bundespräsident Christian Wulff (l) wird am Sonntag (16.10.2011)in Kabul vom afghanischen Präsidenten Hamid Karsai empfangen. Es ist der erste Staatsbesuch eines deutschen Bundespräsidenten am Hindukusch seit 44 Jahren. Foto: Wolfgang Kumm dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais Christian Wulff wa Ujerumani (kushoto) akikutana na Rais Hamid Karzai wa AfghanistanPicha: picture-alliance/dpa

Wulff tayari amekutana na Rais Hamid Karzai wa Afghanistan, kwanza alikuwa na mazungumzo na watetezi wa haki za binadamu hususan wale wanaopigania haki za wanawake kwa ajili ya maandalizi ya mkutano kuhusu Afghanistan uliopangwa kufanyika mjini Bonn Ujerumani hapo mwezi wa Desemba.

Horst Köhler Zapfenstreich
Rais wa zamani wa Ujerumani Horst KöhlerPicha: AP

Hapo mwezi wa Mei mwaka jana, mtangulizi wa Wulff ambaye alikuwa Horst Köhler alivitembelea kwa muda mfupi vikosi vya Jumuiya ya Kujihami vya NATO vilioko kaskazini mwa Afghanistan lakini hakukutana na Karzai. Matamshi yaliotolewa na Köhler kwamba uwekaji wa vikosi vya Ujerumani nchini Afghanistan unaweza kuwa na maslahi ya kiuchumi kwa nchi hii,yalisababisha kujiuzulu kwake.

Ujerumani ina zaidi ya wanajeshi 5,000 waliowekwa nchini Afghanistan. Ziara ya mwisho rasmi iliofanywa na mkuu wa nchi wa Ujerumani nchini Afghanistan ni ile ya Rais Heinrich Lubke hapo mwaka 1967.