1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Timor Mashariki atibiwa nchini Australia

11 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D5fJ

Madaktari wanaomtibu rais wa Timor Mashariki, Jose Ramos Horta, wanaamini atapona kikamilifu licha ya kupigwa risasi tumboni na waasi.

Daktari mkuu wa hospitali ya Royal Darwin amesema hali ya rais Horta inatia moyo lakini majeraha aliyoyapata ni mabaya mno. Aidha daktari huyo amesema saa 24 hadi 48 zijazo zitakuwa muhimu kuamua hatima ya kiongozi huyo.

Rais Horta alipigwa risasi mbili katika sehemu ya juu ya kifua chake na risasi moja tumboni alipokuwa nyumbani kwake nje ya mji mkuu wa Timor Mashariki, Dili.

Kiongozi huyo anaendelea kufanyiwa uchunguzi kubaini upasuaji zaidi anaohitaji kufanyiwa.