1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Lebanon ziarani Ujerumani

B.Braden - (P.Martin)2 Desemba 2008

Rais wa Lebanon Michel Suleiman leo anaanza ziara yake ya Ujerumani.Atakapokutana na viongozi wa Ujerumani majadiliano yao bila shaka yatahusika na ujumbe wa Ujerumani unaosaidia kulinda amani kwenye pwani ya Lebanon.

https://p.dw.com/p/G7qQ
Newly-elected Lebanese President Michel Suleiman, sits on his chair at the Lebanese Presidential palace, in the suburban hills of Baabda southeast of Beirut, Lebanon, Monday, May 26, 2008. President Michel Suleiman walked into the presidential palace Monday, assuming office and beginning the monumental task of uniting a wounded nation and reconciling its rival political factions. (AP Photo/Hussein Malla)
Rais wa Lebanon Michel Suleiman.Picha: AP

Rais Suleiman nchini Lebanon anatazamwa kama ni kiongozi anaeweza kujumuisha jamii mbali mbali.Kiongozi huyo alichaguliwa miezi sita iliyopita baada ya majeribio 19 kutofanikiwa kwa sababu ya kinyanganyiro cha madaraka. Mvutano huo ulikuwa kati ya serikali inayoungwa mkono na nchi za magharibi na upande wa upinzani wa Hezbollah unaelemea upande wa Iran na Syria.

Saudi Arabia ilisaidia kuleta maafikiano kati ya pande hizo mbili hasimu katika mkutano maalum uliyoitishwa Doha nchini Qatar na baadae Suleiman alichaguliwa rais wa Lebanon.Nchini humo,rais si mwanasiasa mtendaji tu bali yeye ni kiongozi anaejumuisha jamii mbali mbali na muhimu zaidi rais ndie anaeliwakilisha taifa zima katika nchi za nje na hilo ni muhimu kwa wote.Kwani kihistoria Lebanon imegawika katika makundi na vyama mbali mbali vya kisiasa na kidini.

Hivi sasa makundi makuu mawili ni kambi ya Waziri Mkuu Fouad Siniora inayoelemea nchi za magharibi na wafuasi wa kundi la Kishia la Hezbollah.Na kila upande unasaidiwa na majirani wa kanda hiyo. Mvutano kati ya pande hizo mbili ulihatarisha kuitumbukiza nchi hiyo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe siku chache tu kabla ya kuchaguliwa kwa Michel Suleiman.

Saudi Arabia ilipoitisha mkutano wa dharura mjini Doha Qatar,makundi hasimu yaliafikiana kuunda serikali ya umoja wa taifa na kupiga marufuku matumizi ya silaha katika migogoro ya ndani na hivyo kufungua njia ya kumchagua Suleiman.Kiongozi huyo,kama rais mpya wa Lebanon amebeba jukumu kubwa la kutenzua migogoro inayoibuka nchini humo.Hapo kuna suala ichukue msimamo gani kuhusu nchi jirani Syria.Je,Israel itazamwe kama ni adui au jirani anaeweza kuwa rafiki?

Rais Suleiman akiyatumia maafikiano ya Doha kufufua majadiliano kati ya makundi hasimu anaamini hiyo ni njia ya kutenzua matatizo yao.Kwa maoni yake matatizo yaliyokuwepo yapatiwe ufumbuzi ili yasije kuripuka upya katika siku zijazo.