1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais mpya wa Ujerumani achaguliwa leo

30 Juni 2010

Leo tarehe 30 Juni 2010, Ujerumani inamchagua rais mpya. Lakini kiongozi huyo wa taifa hachaguliwi moja kwa moja na raia, bali na baraza maalum la Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/O6bd
Niedersachsens Ministerpraesident Christian Wulff (CDU) gibt am Donnerstag, 03. Juni 2010, im Bundestag in Berlin ein Pressestatement ab. Bundeskanzlerin Angela Merkel hat die Kandidatur des niedersaechsischen Ministerpraesidenten Christian Wulff als Nachfolger von Bundespraesident Horst Koehler offiziell bestaetigt. Sie halte ihn fuer einen wunderbaren zukuenftigen Bundespraesidenten, sagte die CDU-Chefin am Donnerstagabend im Beisein der Vorsitzenden von CSU und FDP, Horst Seehofer und Guido Westerwelle. (apn Photo/Jens Schlueter) ***** Joachim Gauck, ehemaliger Bundesbeauftragter fuer die Unterlagen des Staatssicherheitsdienstes der DDR und Kandidat der SPD und der Gruenen fuer die Wahl zum Bundespraesidenten, spricht am Freitag, 04. Juni 2010, in der Bundespressekonferenz in Berlin. (apn Photo/Berthold Stadler)
Wagombea wadhifa wa urais Christian Wulff(kushoto) na Joachim Gauck.Picha: AP

Baraza hilo maalum hujumuisha wabunge wa serikali kuu ya Berlin,wa serikali za majimbo 16 na wajumbe wa kiraia kutoka tabaka mbali mbali za jamii.Kawaida baraza hilo hukutana kila baada ya miaka mitano kumchagua rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani. Lakini, baada ya Horst Köhler kuwa rais wa kwanza kujiuzulu kabla ya kumaliza muhula wake,baraza hilo halina budi kumchagua mrithi wake. Kwani kuambatana na kipengele cha 54 cha Katiba ya Ujerumani, baraza hilo linapaswa kukutana ili kumchagua rais mpya katika kipindi cha siku thelathini kufuatia kujiuzulu kwa rais. Na leo ni siku 30 tangu Horst Köhler alipojiuzulu.

Wajumbe wa kiraia katika baraza hilo maalum, hutokea tabaka mbali mbali za kiraia kama vile fasihi,sanaa au spoti yaani ni watu mashuhuri katika jamii. Wanaweza pia kuwa wanasiasa lakini hilo si lazima. Na baraza hilo linalokutana hivi punde, lina wajumbe 1244. Katika kura zitakazopigwa hii leo kumchagua rasi mpya, serikali kuu ya muungano wa vyama ndugu vya CDU/CSU na chama cha kiliberali FDP inatazamiwa kuwa na uwingi wa kati ya kura 645 hadi 647 kuliko ule uwingi unaohitajiwa kushinda.

Vyama hivyo tawala vimemteua mwanachama wa CDU-Waziri Mkuu wa Jimbo la Niedersachsen, Christian Wulff mwenye umri wa miaka 51, kushika wadhifa wa urais. Kwa upande mwingine, vyama vya upinzani vya SPD na Kijani vinamuunga mkono mwanaharakati wa haki za binadamu wa Ujerumani ya Mashariki ya zamani Joachim Gauck alie maarufu miongoni mwa raia.Yeye ni mgombea huru asie na chama. Ikiwa padri huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 70 atamshinda Wulff, hilo litakuwa pigo kubwa kwa serikali ya Kansela Angela Merkel na hata kusababisha mzozo wa kisiasa.

German Chancellor Angela Merkel addresses a news conference about Germany's budget cuts in Berlin, on Monday, June 7, 2010. The German Cabinet has finalized a package of government savings meant to keep the country's debt in check. Chancellor Angela Merkel says the country needs to save a total of 80 billion euro (US dlrs 96 billion) through 2014. (AP Photo/Markus Schreiber)
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: AP

Umaarufu wa Kansela Merkel umepungua tangu alipochaguliwa tena Septemba iliyopita. Sababu kuu ni migogoro ndani ya serikali yake ya muungano pamoja na vile alivyoukabili mzozo wa kanda inayotumia sarafu ya Euro. Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni na gazeti maarufu la Kijerumani "Bild" umeonyesha kuwa asilimia 48 ya Wajerumani wanamtaka Merkel ajiuzulu ikiwa Wulff alieteuliwa na serikali ya muungano hatochaguliwa rais hii leo. Wanaosema abakie madarakani ni asilimia 30. Nchini Ujerumani,wadhifa wa rais kwa sehemu kubwa ni cheo cha heshima na Horst Köhler alikuwa maarufu miongoni mwa raia - na Wajerumani wanatoa umuhimu nani anaewaakilisha kimataifa.

Mwandishi:D.Scheschkewitz/ZPR/P.Martin/DPA/AFPE

Mhariri,Charo,Josephat