Putin ashutumu mataifa ya magharibi
22 Novemba 2007Matangazo
Rais Vladimir Putin wa Urusi ameshutumu mataifa ya magharibi kwa kuingilia kati siasa za nchi yake.
Wakati wa mkutano wa kampeni ya bunge mjini Moscow kiongozi huyo wa Urusi amesema serikali za kigeni zimekuwa zikidhamini wapinzani wake kuidhoofisha Urusi ili kwamba waweze kutekeleza mbinu zao chafu.Kauli hiyo kali ya Putin inakuja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa bunge la taifa Duma mwezi ujao.
Putin anaongoza kwenye orodha ya wagombea ubunge wa chama cha Muungano wa Urusi ambacho kinaongoza kwa kiwango kikubwa kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni.