1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRISTINA:aliekuwa kiongozi wa waasi adai ushindi Kosovo

18 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIm7

Aliekuwa kiongozi wa waasi katika eneo la Kosovo Hashim Thaci amedai kuwa ameshinda uchaguzi uliofanyika jana.

Ikiwa itakuwa waziri mkuu,Thacki atatangaza uhuru wa Kosovo mwanzoni mwa mwezi desemba.

Hatahivyo idadi ya wapiga kura ilikuwa chini ya asilimia 45 kutokana na wakosovo wenye asili ya Kialbania kufadhaika baada ya viongozi wao kushindwa kuleta uhuru.