Polisi yaua wawili Tanzania | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 06.01.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Polisi yaua wawili Tanzania

Polisi ya Tanzania yathibitisha kuwa watu wawili wamekufa baada ya mapambano kati yake na waandamanaji wa chama kikuu cha upinzani nchini humo, Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kikosi cha Kuzuia Fujo nchini Tanzania

Kikosi cha Kuzuia Fujo nchini Tanzania

Kwa uchache watu wawili wamekufa baada ya kupigwa risasi na Polisi wa Tanzania katika mji wa Kaskazini wa Arusha na wengine wengi wanashikiliwa na jeshi hilo hadi sasa.

Miongoni mwa waliokamatwa na viongozi 10 wa chama cha CHADEMA, akiwemo aliyekuwa mgombea wa urais wa chama hicho katika uchaguzi uliopita, Dkt. Wilbrod Slaa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, pamoja na wabunge wa eneo hilo.

Chanzo cha maandamano hayo ni kuupinga uchaguzi wa meya wa Arusha kwa madai kwamba idadi ya madiwani wanaoviwakilisha vyama vya CCM na CHADEMA inafanana ila walizuiwa kupiga kura. Mwandishi wetu wa Arusha, Nicodemus Ikonko, amekifuatilia kisa hicho na hii hapa taarifa yake.

Mwandishi: Nikodemus Ikonko

Mhariri: Josephat Charo

 • Tarehe 06.01.2011
 • Mwandishi Admin.WagnerD
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/zuEZ
 • Tarehe 06.01.2011
 • Mwandishi Admin.WagnerD
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/zuEZ

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com