1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Kenya yakabiliwa na kibarua kigumu cha kutuliza ghasia za kikbaila na kisiasa

28 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyqY

NAIROBI:

Polisi nchini Kenya inakabiliana na kazi ngumu ya kutuliza ghasia kati ya makabila yanaohasiamiana.Ghasia zilichochewa na uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita. Mapigano ya kikabila yameripotiwa katika miji ya Naivasha na Nakuru .Kwa uchache watu 19 wameuawa katika ghasia za kikabila zilizotokea mwishoni mwa juma katika mkoa wa Bonde la Ufa.Mapigano kati ya kabila la rais Mwai Kibaki la WaKikuyu,dhidi ya waLuo na waKalenjin,ambao wanamuunga mkono kiongozi wa upinzani Raila Odinga,yamesababisha mauaji ya watu zaidi ya 120 tangu Alhamisi.

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa-Koffi Annan,aliewasili nchini humo wiki jana ili kujaribu kupatanisha mgogoro wa kisiasa unaoendelea,ameziomba pande zote katika mzozo wa kisiasa ,kila moja kutaja watu wanne wa kuziwakilisha kwenye mazungumzo.Odinga anasema Kibaki aliibia kura katika uchaguzi wa rais wa Disemba 27 na anailaumu serikali kwa kuyalinda magenge ya vijana yanayofanya mashambulizi kwa raia wasio na hatia.Mapigano ambayo yalianza tangu Kibaki kutangazwa kushinda uchangauzi huo,yamesababisha watu 800 kufa na wengine robo millioni kuachwa bila makazi.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uingereza David Milliband amesema kuwa hatua zinachukuliwa kukomesha ghasia za kisiasa nchini Kenya.