1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UgaidiUjerumani

Ujerumani yaimarisha ulinzi katika Kanisa Kuu la Cologne

30 Desemba 2023

Mamlaka nchini Ujerumani ziko katika hali ya tahadhari kufuatia kitisho cha kushambuliwa Kanisa Kuu la mjini Cologne katika siku ya mkesha wa mwaka mpya.

https://p.dw.com/p/4aizm
Deutschland | Polizeieinheiten am Kölner Dom
Polisi wakiimarisha ulinzi katika Kanisa Kuu mjini Cologne, Ujerumani: 23.12.2023Picha: Ina Fassbender/AFP/Getty Images

Polisi wameimarisha ulinzi katika Kanisa hilo baada ya kupokea taarifa kuhusu uwezekano wa kufanyika mashambulizi ya kigaidi.

Kanisa hilo ambalo ni moja ya majengo ya kale na alama muhimu nchini Ujerumani limezuia kupokea watalaai hivi sasa. Afisa mkuu wa eneo la magharibi mwa Ujerumani Martin Lotz amesema hatua hizo za kiusalama zinalenga kuzuia shambulio lolote kama hilo bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi. Mwanaume mmoja anashikiliwa na polisi akishukiwa kupanga shambulio dhidi ya Kanisa hilo la Cologne.

Lotz ameonya kuwa maafisa watakuwa na silaha nzito na kusema kuwa hilo ni muhimu ili kuhakikisha usalama wa raia wakati huu wa sikukuu. Hata hivyo hatua hii ya kuimarisha usalama imetokana pia na matukio ya vurugu yaliyoshuhudiwa kote Ujerumani katika mkesha wa mwaka mpya wa 2022.