Polisi nchini Syria washambulia wanaharakati
24 Aprili 2011Polisi waliokuwa wamevaa nguo za kawaida na wakibeba silaha, walivamia baadhi ya nyumba katika kitongoji cha Harasta na waliwakamata wanaharakati.
Vikosi vya usalama na wafuasi wa Rais Assad waliobeba silaha, waliwaua takriban watu 112 katika siku mbili zilizopita baada ya siku ya Ijumaa kuwafyatulia risasi waandamanaji wanaodai uhuru wa kisiasa na baadaye katika mazishi ya watu hao yaliyofanyika jana.
Wakati huohuo, wabunge wawili kutoka katika mji wa Deraa wamejiuzulu kupinga mauaji hayo yaliyofanywa na jeshi.
Kiongozi wa kidini katika mji huo pia amejiuzulu kupinga ghasia hizo. Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani, imewatahadharisha raia wake kuepuka kufanya safari nchini Syria, iwapo itawezekana, na pia kuwashauri raia wake walioko nchini humo kuondoka.