Idadi ya watu waliouawa katika maandamano ya kudai mageuzi ya demokrasia nchini Syria imeongezeka hadi kufikia 88.
Rais wa Syria Bashar Assad
Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limetoa takwimu hizo kuuambatana na ripoti za wanaharakati wa nchi hiyo.
Hiyo jana, vikosi vya usalama vya Syria vilifyatulia risasi na mabomu ya kutoa machozi katika mikutano ya upinzani iliyokuwa ikifanyika nchi nzima.
Waandamanaji nchini Syria
Kuendelea huko kwa maandamano ni dalili kwamba jaribio la Rais wa nchi hiyo Bashar al Assad kuzima upinzani huo uliodumu kwa mwezi mmoja na kusababisha machafuko pamoja na ahadi alizotoa za kufanya marekebisho, limeshindwa.
Rais al Assad na vyombo vya habari vya taifa, vimeendelea kulaumu njama zinazofanywa kusababisha machafuko katika maandamano hayo ya upinzani.
Waandamanaji Yemen
Wakati huohuo, nchini Yemen nako, maelfu ya watu walikusanyika katika mitaa ya mji mkuu Sanaa na mji wa Taiz hapo jana katika maandamano ya kumpinga rais wa nchi hiyo Ali Abdullah Saleh.