PHILADELPHIA:Obama ataka Marekani iachane na Iraq
23 Mei 2007Matangazo
Barak Obama anayewania kuteuliwa na chama cha Demokratic kugombea urais wa Marekani, amesema kuwa nchi hiyo inatakiwa kujiondoa nchini Iraq na kushughulikia matatizo yake ya ndani.
Obama, Seneta kutoka jimbo la Illinois, yuko nyuma ya Hillary Clinton kwa mujibu wa kura za maoni kuweza kupata uteuzi huo.
Obama ambaye baba yake ni Mkenya, amesema kuwa vita ya Iraq, ni moja kati ya makosa makubwa ya mikakati katika historia ya kijeshi nchini Marekani.