1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PESHAWAR:Mlipuko wa bomu waua wawili na kujeruhi watano

9 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBKL

Wanajeshi wawili wameuawa na wengine watano kujeruhiwa pale bomu lilipolipuka kwenye eneo la kaskazini magharibi mwa Pakistan linalokabiliwa na wanamgambo.Tukio hilo limetokea katika mlipuko mjini Karbala kwa mujibu wa msemaji wa jeshi Meja Jenerali Waheed Arshad .

Kulingana na wakazi wa eneo hilo bomu hilo lilitungwa kwenye daraja moja mjini Karbala karibu na mji mkubwa wa Mingora.Wakati huohuo Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto anatoa wito kwa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kumshinikiza Rais Pervez Musharraf aliyetangaza hali ya hatari mwishoni mwa juma lililopita aidha kuagiza polisi waliojihmi kuzingira nyumba yake na kumzuia kutoka.

Wafuasi wake 5,000 wanaripotiwa kukamatwa na polisi ili kuzuia mkutano wa hadhara kufanyika ili kupinga hali ya hatari iliyotangazwa mwishoni mwa juma lililopita.Kulingana na uongozi mikutano ya hadhari imepigwa marufuku katika hali ya hatari .Mkutano wa Bi Bhutto ulipangwa kufanyika mjini Rawalpindi hii leo.Kwa mujibu wa meya wa mji huo ripoti ya kuaminika inaeleza kuwa huenda walipuaji wa kujitoa muhanga wanaandaa kushambulia mkutano huo.Rais Musharraf bado anawabana wapinzani wake hata baada ya kutangaza kuwa uchaguzi utafanyika mwezi Februari ikiwa ni mwezi mmoja baada ya tarehe iliyowekwa awali.

Tangazo hilo linatolewa baada ya shinikizo kutoka kwa Marekani iliyo mwandani wake mkuu wa kimataifa.Polisi waliwashambulia wafuasi yapata 300 wa Bi Bhutto walipokusanyika ili kufunga safari ya Rawalpindi na kuwakamata 25.