1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS:Sheria za uhamiaji kuwa ngumu zaidi

Bunge nchini Ufaransa linaidhinisha hatua ya kufanya uchunguzi wa shanga za urathi kwa wahamiaji wanaotaka kuungana na familia zao nchini humo.Bunge dogo nchini humo aidha linaidhinisha sheria inayobana zaidi uhamiaji nchini humo ambayo inawalazimu wahamiaji hao kujua lugha ya Kifaransa aidha maadili ya nchi hiyo.Sheria hiyo iliyoandaliwa na waziri wa uhamiaji wa Ufaransa Brice Hortefeux inawekea jamaa za wahamiaji masharti mapya yanayojumisha ujuzi wa lugha ya Kifaransa na hakikisho la pesa za matumizi.

Hata hivyo mabadiliko hayo yanatilia mkazo uchunguzi wa shanga za urathi utakaofanyika kwa hiari na kuelezwa kuwa majaribio mpaka ifikapo mwisho wa mwaka 2010.Hatua hiyo inachukuliwa kwa wahamiaji wasiokuwa na maelezo ya kutosha kuhusu uraia wao.

Kwa mujibu wa serikali wahamiaji hao watarejeshewa gharama za uchunguzi huo endapo maombi yao yanafanikiwa.Waziri wa uhamiaji aidha anapanga kuunda tume maalum itakayotathmini utekelezaji wa shughuli nzima kila mwaka.Serikali ya Ufaransa inalenga kuwarejesha nyumbani kwao wahamiaji haramu alfu 25 ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com