1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Kampeni za kugombea urais zaanza rasmi

9 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCB6

Kampeni za uchaguzi wa rais nchini Ufaransa zimeanza rasmi hii leo wiki mbili kabla ya kufanyika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais.

Kura ya maoni inaonyesha kuwa mgombea wa chama cha kihafidhina cha UMP Nicolas Sarkozy na msoshalisti Segolene Royal wako mstarti wa mbele katika kinyang’anyiro hicho.

Mgombea wa chama mrengo wa kadiri Francois Bayrou na mgombea wa mrengo wa kulia Jean-Marie Le Pen pia wanaungwa mkono katika uchaguzi huo.

Wagombea 12 wanatetea kuchukua kiti cha urais baada ya rais Jacque Chirac mwenye umri wa miaka 74 kutangaza kuwa hatawania tena wadhfa wa urais pindi muda wake utakapo kamilika.