PARIS: watoto lazima walindwe katika sehemu za mizozo ya kivita | Habari za Ulimwengu | DW | 06.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS: watoto lazima walindwe katika sehemu za mizozo ya kivita

Wawakilishi kutoka nchi 60 wanakutana mjini Paris, Ufaransa kuzungumzia juu ya njia thabiti za kuwalinda watoto katika sehemu zinazokabiliwa na mizozo ya kivita.

Kwa mujibu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, watoto wapatao laki mbili na nusu wanatumiwa kama askari katika sehemu mbalimbali za mizozo duniani. Akizumngumza kwenye mkutano huo waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani bibi Wiezcorek Zeul ameulezea uovu wa kuwatumia watoto kama askari kuwa ni aina mbaya sana ya utumwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com