PARIS: Sheria kali za uhamiaji zaidhinishwa Ufaransa | Habari za Ulimwengu | DW | 21.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PARIS: Sheria kali za uhamiaji zaidhinishwa Ufaransa

Bunge la Ufaransa limeidhinisha mswada unaopendekeza kuwa na sheria kali zaidi kwa baadhi ya wahamiaji.Chama tawala cha kihafidhina cha UMP kimeungwa mkono na New Centre Party kupitisha sheria hiyo.Kuambatana na sheria hiyo,wahamiaji watapaswa kujifunza lugha ya Kifaransa na kutoa ushahidi wa kuweza kujitegemea kifedha,kabla ya kuruhusiwa kuungana na familia ambazo tayari zinaishi Ufaransa.Sheria hiyo mpya vile vile itaruhusu kuwafanyia uchunguzi wa DNA, ili kuhakikisha wale wanaoomba viza za uhamiaji, kweli wanahusiana kindugu na wakazi wa Ufaransa wanaofuatwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com