1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS :Merkel na Chirac wana imani na kampuni ya Airbus

13 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3O

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na rais Jacques Chirac wa Ufaransa wamesema,nchi hizo mbili zigawane sawa sawa athari za mageuzi yaliopangwa kufanywa katika kampuni ya Airbus inayotengeneza ndege barani Ulaya.Rais Chirac amesema,ufunguo wa mafanikio ni kwa viwanda vya Toulouse na Hamburg kugawana sawa sawa mzigo wa mageuzi yatakayofanywa.Baada ya mkutano wake na Kansela Merkel,Chirac alisema,ana imani kuwa kampuni ya Airbus itafanikiwa kusuluhisha mzozo wa sasa wa kuchelewa kuwasilisha ndege zake mpya aina ya super jumbo-A380.Kansela Merkel nae amesema,Airbus inaungwa mkono na Ujerumani kama mradi muhimu wa kiviwanda,lakini hakueleza ikiwa serikali yake ipo tayari kuisaidia kifedha kampuni hiyo yenye matatizo.