1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Mbunge atimuliwa kwa kauli za kibaguzi

28 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXH

Chama cha upinzani cha Kisoshalisti nchini Ufaransa kimemtimuwa mbunge mwandamizi wa chama hicho kwa kurudia kutowa matamshi ya kibaguzi.

Georges Freche kiongozi wa baraza la mkoa kusini mwa Ufaransa amekuwa akilalamika mara kadhaa kwamba kuna wachezaji wengi mno weusi katika timu ya soka ya Ufaransa. Hapo Alhamisi alitozwa faini ya euro 15,000 kutokana na kuwatukana na kuwaita binaadamu wenye mapungufu Waalgeria waliopigana kwa upande wa Ufaransa wakati wa vita vya kupigania uhuru wa nchi yao.

Freche ni mfuasi wa mgombea urais Segolene Royal lakini matamshi yake yamekuwa tahayuri kwa chama ikiwa imebakia miezi mitatu tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Ufaransa.