1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Benedikt ziarani Ujerumani

Martin,Prema/zpr22 Septemba 2011

Papa Benedikt wa 16 leo anaanza ziara yake rasmi ya siku nne nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/Rn4p
Pope Benedict XVI blesses the faithful during the "Urbi et Orbi" (to the City and to the World) message in St. Peter's square at the Vatican, Saturday, Dec. 25, 2010. Pope Benedict XVI in his Christmas Day message Saturday urged Catholics loyal to him in China to courageously face limits on religious freedom and conscience. (AP Photo/Andrew Medichini)
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedikt XVIPicha: AP

Baada ya kupokewa na Rais Christian Wulff na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani atakuwa na mazungumzo pamoja na wanasiasa hao wawili. Mchana atahutubia bunge la Ujerumani - jambo lililozusha mabishano nchini humu. Leo jioni atasoma misa katika uwanja mkubwa wa michezo jijini Berlin na zaidi ya watu 70,000 wanatazamiwa kushiriki katika misa hiyo.

Miji mingine itakayotembelewa na Papa Benedikt ni Erfurt, Thüringer Eichsfeld na Freiburg. Ulinzi wa usalama umeimarishwa katika miji hiyo yote mpaka siku ya Jumapili. Hii ni ziara ya tatu kufanywa na Papa Benedikt nyumbani kwake Ujerumani tangu alipochaguliwa kiongozi wa Kanisa Katoliki katika mwaka 2005 na ni ziara yake ya kiserikali ya kwanza nchini humu.