OUGADOUGOU: Gbagbo na Soro kutia saini makubaliano ya amani ya Ivory Coast | Habari za Ulimwengu | DW | 04.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

OUGADOUGOU: Gbagbo na Soro kutia saini makubaliano ya amani ya Ivory Coast

Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast na kiongozi wa waasi Guillaume Soro leo hii wanatia saini makubaliano yenye lengo la kukomesha mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe nchini humo.Makubaliano hayo yalipatikana siku ya Jumamosi chini ya usimamizi wa Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso.Desemba mwaka jana,Rais Gbagbo alipendekeza kuwa na mazungumzo ya uso kwa uso kwa azma ya kuzindua utaratibu wa amani katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com