OTTAWA: Serikali ya Canada kumlipa fidia Maher Arar aliyezuiliwa kimakosa kwa tuhuma za ugaidi. | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

OTTAWA: Serikali ya Canada kumlipa fidia Maher Arar aliyezuiliwa kimakosa kwa tuhuma za ugaidi.

Serikali ya Canada imekubali kumlipa raia wa nchi hiyo mzaliwa wa Syria fidia ya Euro karibu milioni sita nukta tisa kwa kumtuhumu kimakosa kwa ugaidi.

Maher Arar alikaa gerezani nchini Syria kwa muda wa mwaka mmoja ambapo anadai aliteswa kabla ya kuhamishiwa Marekani mwaka 2002.

Maher Arar alikamatwa katika uwanja wa ndege wa John F. Kennedy mjini New York alipokuwa akirejea nchini Canada kutoka likizoni.

Waziri Mkuu wa Canada, Stephen Harper alimtaka radhi hadharani Maher Arar ambaye ingawa aliridhia lakini alisema maisha yake yamevurugika tangu alipokamatwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com