1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ocampo kufungua kesi za washukiwa wa machafuko nchini Kenya wiki mbili zijazo

Josephat Nyiro Charo2 Desemba 2010

Majina ya watu sita raia wa Kenya wanaotuhumiwa kuhusika na kuipanga njama iliyosababisha ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu uliopita yatabainika katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

https://p.dw.com/p/QOJM
Luis Moreno Ocampo, muendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya ICCPicha: AP

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC,Luis Moreno Ocampo,kesi mbili zitawasilishwa ifikapo tarehe 17 mwezi huu kwa minajili ya kuyatathmini na kuyadurusu maelezo yaliyopo na ushahidi uliokusanywa mpaka sasa.Mwanasheria huyo aliyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo alasiri mjini Nairobi.Hata hivyo alifafanua kuwa ijapokuwa majina ya watuhumiwa hao yatajulikana,sharti sheria ifuate mkondo wake ndipo hatma yao iwe bayana.

Kwa upande mwengine,mpatanishi Dr Koffi Annan wa zamani katika mzozo wa kisiasa uliotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 uliogubikwa na utata amewalaumu viongozi wa Kenya kwa kutowajibika ili kuwatia hatiani wahalifu waliosabisha ghasia hizo.