NOUKCHOUT : Kampeni za uchaguzi zafanyika kwa utulivu | Habari za Ulimwengu | DW | 05.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NOUKCHOUT : Kampeni za uchaguzi zafanyika kwa utulivu

Kampeni katika uchaguzi wa bunge na mabaraza ya miji zimeanza kwa utulivu hapo jana zikiwa kama historia katika kupiga hatua ya demokrasia nchini Mauritania tokea mapinduzi ya kijeshi hapo mnwezi wa Augusti mwaka 2005.

Imeelezwa kwamba kulikuwa hakuna repoti ya matukio ya vurugu na kwamba kila kitu kilikwenda kwa utulivu.

Hata hivyo Mkuu wa kundi la watazamaji wa uchaguzi la Umoja wa Ulaya Marie- Anne Isler Beuguin amesema kwamba Wamauritania wameendelea kuwa na mashaka ambayo inabidi yashughulikiwe ili kuweza kufanikisha uchaguzi huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com