Niedecken Mjini Bonn:Haki na muziki kwenye meza moja
3 Septemba 2010Kwani ndoto ya mwimbaji huyo wa bendi ya BAP kutoka mji wa Cologne ni kuwa na ulimwengu wa haki na katu hatoachana na ndoto hiyo.Wimbo unaoitwa,"Ingelikuwa Vizuri" unaeleza kuwa hakuna anayelazimika kuwa na njaa,hakuna anaeteseka,hakuna bahili,mwenye nacho atagawa bila ya shaka na hakutakuwepo tena sababu za ugaidi,chuki na kuoneana wivu."
Balozi wa Afrika
Kuna baadhi ya watu wanaomkosoa mwimbaji huyo wa BAP kwa kuwa mtu mwema kupindukia.Lakini hiyo wala haimsumbui. Katika mahojiano yake na gazeti moja miaka michache iliyopita aliuliza, iwapo awe mtu mbaya eti kwa vile wapo wanaokerwa na harakati zake za kupinga dhulma duniani? Mara kwa mara Wolfgang Niedecken ameeleza kwanini hawezi kuachana na mada ya askari watoto na Uganda, hasa kufuatia ziara yake nchini humo katika mwaka 2004. Wakati huo, alikuwa ziarani barani Afrika pamoja na waandishi wa habari kama "balozi kwa bara la Afrika" - Akieleza hisia zake anasema,''Nilishudia kwa macho yangu mwenyewe huko kaskazini ya Uganda na nikaamua kuishughulikia mada hiyo. Lakini mara ya kwanza kabisa nilikuwepo Msumbiji - hiyo ilikuwa miaka 20 iliyopita."kuhusu askari watoto.
Askari watoto wa Uganda
Kwa hivyo, mwaka huo wa 2004 ambapo Uganda ilikuwa ikipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe,Niedecken aliamua kuwashughulikia askari watoto.Wakati wa ziara hiyo Niedecken alikutana na wasichana wawili katika kituo kinachowasaidia askari watoto wa zamani kurejea katika maisha ya kawaida. Watoto hao walitekwa nyara,walizuiliwa kama watumwa na walibakwa na waasi mara kwa mara. Baadae wasichana hao na watoto wao walipata Ukimwi. Yaliyowafika wasichana hao yalimhuzunisha sana na wakati huo akashindwa hata kuendelea na mahojiano yake na timu ya televisheni iliyofuatana nae katika ziara yake barani Afrika.
Picha na Muziki
Niedecken si mwanamuziki tu bali ni mchoraji pia.Yeye amesomea uchoraji na picha zake zimewahi kuonyeshwa katika majumba ya sanaa nchini Ujerumani.Na muziki wake unajulikana kama ni wa midundo ya rock ya lahaja ya Kölsch yaani kutoka kanda ya Cologne.
Kwa njia fulani nyimbo zake zina ujumbe wa kisiasa na hata hisia za binafsi. Mwanamuziki Niedecken daima amepigania haki.Kwa mfano mwaka 1992,wageni waliposhambuliwa na wanazi mamboleo, Niedecken alitayarisha tamasha lililowaleta pamoja wanamuziki na mashabiki kuwapinga wafauasi wa sera kali za mrengo wa kulia.Sasa anashughulikia bara la Afrika. Anasema ameanzisha mradi maalum "Rebound" unaosaidia kuzijenga upya shule huko kaskazini ya Uganda.Kutakuwepo mabweni ili wanafunzi waweze kuishi huko wakati wa maosmo. Lengo ni kuwapa askari watoto wa zamani nafasi ya kujielimisha na kuanza maisha mapya.
Lakini hii leo,wageni mashuhuri na wasio mashuhuri watakapokutana mjini Bonn, Wolfgang Niedecken anataka kuwatumbuiza kwa muziki wake.
Mwandishi: Prema Martin-/ZPR-Görtz,Birgit
Mhariri: Othman,Miraji