1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEWYORK:UN yaridhia vikosi kwenda Chard na Afrika ya Kati

26 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMf

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limeridhia kupelekwa kwa jeshi la Umoja wa Ulaya na askari polisi wa Umoja wa Mataifa katika nchi za Chard na Jamhuri ya Afrika ya Kati kulinda usalama wa raia waliyoathirika na mzozo wa Darfur.

Mawaziri wa Ulinzi wa Umoja wa Ulaya wiki iliyopita waliridhia kupelekwa kwa kikosi cha askari elfu 4 wengi wakiwa ni wa kutoka Ufaransa ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kuna wakimbizi kiasi cha laki sita katika nchi hizo.