NEWYORK:Nchi za Magharibi zatka hatma ya Kosovo itangazwe haraka | Habari za Ulimwengu | DW | 10.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEWYORK:Nchi za Magharibi zatka hatma ya Kosovo itangazwe haraka

Nchi za magharibi zimelitaka baraza la usalama la Umoja wa mataifa kutoa uamuzi wake juu ya hatma ya uhuru wa jimbo la Kosovo katika kipindi cha wiki moja ijayo. Hata hivyo kiongozi wa baraza hilo China imesema mataifa yenye nguvu bado yamegawika juu ya suala hilo.Waziri mkuu wa Kosovo ameitolea mwito Marekani kutoa tarehe ya kutangazwa uhuru kwa jimbo hilo.Jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO imesema watu wa Kosovo lazima wapewe ahadi ya kupata uhuru wa jimbo lao haraka iwezekanavyo la sivyo wakaazi hao ambao ni waalbania watazusha hasira.Urusi ambayo inashikilia kura ya turufu kwenye baraza la usalama haiwezi kukubali uhuru kwa Kosovo bila idhini ya mshirika wake wa Karibu Serbia ambayo inapinga vikali hatua hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com