New York.Wapalestina waijia juu Israel huko Umoja wa Mataifa.
10 Novemba 2006Matangazo
Wapalestina wameutaka Umoja wa Mataifa uingilie kati haraka kufuatia mashambulio ya Israel kaskazini mwa Gaza.
Muakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour amedai uchunguzi ufanywe wa mashambulio ya Beit Hanoun ambako raia 18 waliuliwa Jumatano iliyopita.
Jeshi la Israel linadai, tukio hilo limesababishwa na makosa ya kiufundi katika zana zao za kijeshi.