1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK.Wanachama wajadili hatua za kuiwekea Iran vikwazo

3 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwT

Nchi tano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa na Ujerumani zinafanya majadiliano kuhusu hatua ya kuiwekea vikwazo Iran juu ya mpango wake wa nyuklia.

Mazungumzo hayo yamefanyika siku moja tu baada ya Iran kutekeleza zoezi la kijeshi lililohusisha makombora yenye uwezo mkubwa.

Watallam wa silaha wamesema kwamba makombora matatu ya Shahab ya Iran yana uwezo wa kushambulia kwa umabli wa hadi kilomota 2000 na hiyo inamaanisha makombora hayo yanaweza kuishambulia Israel au hata Ghuba ya Uajemi.

Iran ilitekeleza zoezi la kijeshi siku moja baada ya Marekani kufanya zoezi la aina hiyo na kuzindua mikakati ya kuzuia usafirishaji wa silaha za maangamizi makubwa.