1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:UNICEF yasema hali ya watoto Iraq ni mbaya

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBz3

Shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa UNICEF, limesema kuwa zinahitajika kiasi cha dola millioni 42 kwa ajili ya kuwasaidia watoto nchini Iraq

Katika taarifa yake UNICEF imesema kuwa hali ya watoto nchini Iraq imefikia katika hatua mbaya.

Taarifa hiyo imeonya kulipuka kwa magonjwa ya kuhara katika msimu wa joto, kutokana na idadi kubwa ya watoto nchini humo kutokuwa na uwezo wa huduma ya maji safi.

UNICEF imesema kuwa kiasi hicho cha fedha kitatumika kwa ajili ya watoto waliyoko nchini Iraq pamoja na wale waliyokimbilia katika nchi za Jordan na Syria