NEW YORK:Umoja wa Mataifa watahadharisha juu ya hatari ya njaa katika eneo la Sahel
10 Oktoba 2006Matangazo
Mamilioni ya watoto wanakabiliwa na tishio kubwa la kufa njaa katika nchi zinazopakana na jangwa la Sahara.
Umoja wa Mataifa umetaarifu hayo na kueleza kuwa watoto milioni moja na laki mbili na nusu wenye umri wa chini ya miaka mitano hawapati chakula cha kutosha nchini Niger,Mali, Mauritania na Burkina Faso.
Umoja wa Mataifa umesema msaada wa haraka wa dola milioni hamsini unahitajika kwa ajili ya watoto hao katika nchi hizo.