1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK.katibu mkuu Koffi Annan amelaani mashambulio dhidi ya raia wa Darfur

3 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwU

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Koffi Annan amelaani mashambulio dhidi ya kambi za wakimbizi katika eneo la Darfur magharibi mwa Sudan yanayotekelezwa na wanamgambo wa nchi hiyo.

Annan ameitaka serikali ya Khartoum kuchukua hatua za kuzuia mashambulio hayo dhidi ya raia.

Katika miezi michache iliyopita hali ya machafuko imeongezeka katika jimbo la Darfur.

Takriban watu laki mbili wameuwawa tangu mapigano ya mwaka 2003 na zaidi ya watu milioni mbili wamelazimika kuyahama makaazi yao.