1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK.katibu mkuu ahoji hali ya usalama katika mashariki ya kati

13 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjf
Somalia, tishio la kigaidi
Somalia, tishio la kigaidiPicha: AP

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa anaeondoka Koffi Annan ameeleza kuwa hali ya usalama ni mbaya zaidi katika mashariki ya kati.

Matamshi hayo ni miongoni mwa matamshi ya mwisho mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa mjini New York.

Katibu mkuu amesema Waisrael na Wapalestina wote wamechangia hali hiyo.

Amezitaka nchi zilizo mstari wa mbele katika maswala ya Mashariki ya Kati zikiwa ni pamoja na Marekani, nchi za Umoja wa Ulaya, Urusi na umoja wa mataifa zitafute njia za kuleta amani katika eneo hilo.