1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Walinda amani 180 wachukuliwa hatua za nidhamu

1 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnr

Umoja wa Mataifa umesema kwamba karibu wanajeshi 180,raia na polisi wakiwa katika shughuli za kulinda amani za Umoja wa Mataifa wamechukuliwa hatua za kinidhamu tokea mwanzoni mwa mwaka 2004 kutokana na kuhusika na udhalilishaji wa kingono.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema licha ya sera ya Umoja wa Mataifa kutokuwa na subira kwa vitendo hivyo unyonyaji kwa kutumia ngono na dhuluma unaofanywa na wafanyakazi wa shughuli za kulinda amani wa Umoja wa Mataifa unaendelea kutokea.Tokea mwezi wa Januari mwaka 2004 Umoja wa Mataifa umewachunguza wafanyakazi wake 319 katika shughuli zote za kulinda amani za Umoja wa Mataifa.

Chini ya sheria ya kimataifa sehemu kubwa ya watu wanaotumika kwenye operesheni za kulinda amani hawawezi kuchukuliwa hatua za nidhamu na mfumo wa Umoja wa Mataifa kwa sababu wanakuwa chini ya mamlaka ya nchi zao wenyewe.