1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Wairaki wengi wanaishi katika hali ya umaskini

Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi uliofanywa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, takriban thuluthi moja ya Wairaki wanaishi katika hali ya umaskini huku asilimia tano ya Wairaki wote wakiishi katika umaskini uliokithiri. Aidha ripoti hiyo inasema Wairaki wengi hawafaidi kutokana na utajiri mkubwa wa mafuta wa nchi yao.

Waandishi wa ripoti hiyo wanailaumu Marekani kwa kujaribu kuanzisha soko la kiuchumi kwa haraka. Ripoti ya aina hiyo ni ya kwanza tangu uvamizi wa Irak ulioongozwa na Marekani na imeatayarishwa kutumia data za mwaka wa 2004.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com