1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Shirika la Chakula kuongozwa tena na Mmarekani.

8 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuu

Mwanadiplomasia wa Marekani Josette Sheeran amechaguliwa kuongoza Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP.

Ameidhinishwa kushika wadhifa huo na shirika hilo lenye makao yake makuu mjini Rome hapo Jummane na atachukuwa nafasi ya mwananchi mwenzake wa Marekani aliekuwa akihikilia wadhifa huo James Morris kwa kipindi cha miaka mitano.

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP linatowa misaada ya chakula kwa wastani wa watu maskini milioni 90 zaidi ya nusu ya watu hao wakiwa ni watoto duniani kote.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kabisa takriban watu 25,000 wanakufa kila siku kutokana na matatizo yanayosababishwa na njaa.