1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Makubaliano yafikiwa kukiimarisha kikosi cha Umoja wa Afrika huko Darfur

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAu

Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na serikali ya Sudan zimefikia uamuzi wa kukiimarisha kikosi cha Umoja wa Afrika kinacholinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Walinda amani wa Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur watasaidiwa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa, polisi na vifaa vya urubani.

Naibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa, Marie Okabe, amesema mkutano uliofanyika Jumatatu iliyopita mjini Addis Ababa, Ethiopia ulifikia makubaliano ya kupeleka msaada mkubwa kwa kikosi cha Umoja wa Afrika huko Darfur ikiwa ni pamoja na maofisa zaidi ya 3,000 wakiwemo wanajeshi, polisi na wafanyakazi wengine.

Umoja wa Mataifa ulikubaliana na serikali nya Sudan mwezi Novemba mwaka jana juu ya mpango wa awamu tatu wa kukiimarisha kikosi cha Umoja wa Afrika ikiwa ni pamoja na kupelekwa kikosi cha jeshi la Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa chenye wanajeshi 17,000 na polisi 3,000.

Lakini rais wa Sudan, Omar el Bashi, amekuwa akiyatilia guu makubaliano hayo.