NEW YORK: Kofi Annan amesifu misaada ya China kwa Afrika | Habari za Ulimwengu | DW | 05.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Kofi Annan amesifu misaada ya China kwa Afrika

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan amefurahia tangazo la China la kuongeza maradufu msaada wake kwa bara la Afrika hadi ifikapo 2009. China ilitoa tangazo hilo kwenye mkutano wa ushirikiano wa China na Bara Afrika mjini Beijing.Afisa wa Umoja wa Mataifa amesema,nchi za Kiafrika zikionyesha upya uamuzi wa kupambana na changamoto za bara hilo,sasa zinaweza kunufaika kutokana na ujuzi wa China kuendeleza uchumi na kupunguza umasikini.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com