NEW YORK: Katibu mkuu aliyoteuliwa kwenye Umoja wa matifa Ban Ki-Moon atangaza mipango yake | Habari za Ulimwengu | DW | 24.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Katibu mkuu aliyoteuliwa kwenye Umoja wa matifa Ban Ki-Moon atangaza mipango yake

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa alioteuliwa hivi karibuni Ban Ki-Moon, ametangaza mipango yake ya mageuzi kwenye Umoja wa mataifa ili kurejesha imani kwa taasisi hiyo ya kimataifa. Waziri wa mambo ya kigeni wa Korea Ban Ki-Moon ambae atakabidhiwa mamlaka ya uongozi wa Umoja wa mataifa ifikapo tarehe 1 Januari mwaka ujao, amesema kitu cha kwanza atakachotilia kipau mbele ni kujenga uungaji mkono ili aweze kusonga mbele katika sera zake.

Katibu mkuu wa sasa, Kofi Annan, ataacha kazi hiyo tarehe 31 Disemba mwaka huu baada ya kumaliza mihula miwili ya miaka mitano.

Ban Ki-Moon, ametangaza mipango yake katika hotuba ya kuadhimisha siku kuu ya Umoja wa mataifa ambayo iliwekwa katika kumbukumbu za uundwaji wa taasisi hiyo ya kimataifa mwaka wa 1945. Ban amesema juhudi zake zitaelekezwa juu ya mageuzi katika sekreteriate ya Umoja wa mataifa, kuweka mambo wazi na uhasibu bora.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com