1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ban Ki-Moon anakaribia kushika nafasi ya Kofi Annan

13 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3F

Waziri wa mambo ya kigeni wa Korea Ban Ki-Moon, anatarajiwa kuidhinishwa na Baraza la usalama la Umoja wa mataifa baadae leo kama katibu mkuu mpya wa Umoja wa mataifa kushika nafasi ya Kofi Annan ambae mhula wake unamalizika ifikapo tarehe 31 Disemba mwaka huu. Uteuzi wa Ban Ki-Moon, mwenye umri wa miaka 62, utaidhinishwa na baraza kuu la wajumbe wa nchi 192 bila mjadala wowote.