New Delhi. Karzai aomba msaada zaidi wa kimataifa kupambana na Taliban. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

New Delhi. Karzai aomba msaada zaidi wa kimataifa kupambana na Taliban.

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ameonya kuwa hali ya machafuko nchini humo inaleta kitisho dhidi ya eneo lote. Akizungumza katika mkutano wa kiuchumi juu ya kuijenga upya Afghanistan unaofanyika nchini India , Karzai ametoa wito kwa msaada zaidi wa jumuiya ya kimataifa katika kupambana na wapiganaji wa Taliban.

Waziri mkuu wa India Manmohan Singh ameongezea nguvu wasi wasi huo wa Karzai, kwa kusema kuwa amani nchini Afghanistan ni muhimu kwa ajili ya eneo hilo pamoja na usalama wa dunia.

Mkutano huo unaofanyika mjini New Delhi unahudhuriwa na maafisa wa eneo na wawakilishi kutoka mataifa tajiri ya G8, taasisi za fedha za kimataifa na umoja wa mataifa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com