Neu Ulm Ujerumani. El Masri akamatwa kwa kutuhumiwa kuchoma moto duka! | Habari za Ulimwengu | DW | 18.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Neu Ulm Ujerumani. El Masri akamatwa kwa kutuhumiwa kuchoma moto duka!

Aliekuwa mahabusu kwenye jela ya Marekani ya Guantanamo amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuchoma moto duka moja katika mji wa Neu Ulm kusini mwa Ujerumani.

Mtuhumiwa huyo bwana Khaled el Masri aliwekwa rumande katika duka hilo, na polisi imesema kuwa baadae alipelekwa kwa daktari wa akili ili kufanyiwa uchunguzi.

Bwana el Masri aliefungwa katika jela ya Guantanamo alidai kuwa alitekwa nyara na maafisa wa shirika la ujasusi la Marekani CIA nchini Macedonia na kupelekwa Afghanistan na baadae Guantanamo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com