Netanyahu anataka kukutana ana kwa ana na Abbas
20 Septemba 2011Matangazo
Taarifa hiyo imetolewa na ofisi ya waziri mkuu wa Israel. Netanyahu anatoa mwito kwa serikali ya Wapalestina kurejea katika majadiliano ya ana kwa ana kutafuta suluhisho la amani. Hapo awali, Waziri Mkuu Netanyahu, aliwaonya Wapalestina kuwa amani haiwezi kupatikana kwa kuchukua hatua ya upande mmoja katika Umoja wa Mataifa.
Wakati huo huo, Rais wa Wapalestina Abbas amesisitiza dhamira yake ya kuwasilisha ombi la uanachama kamili, katika Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa.Tangazo hilo limezusha wasiwasi katika jumuiya ya kimataifa. Waziri wa Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle amezihimiza pande zote mbili kurejea katika meza ya majadiliano.